Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul Islam wal Muslimin Mirhashem Husseini aliyasema hayo katika hafla ya usiku wa kuadhimisha kuzaliwa Bibi Zainab al-Kubra (s.a), iliyofanyika katika ukumbi wa Imam Khomeini (r.a), ndani ya Haram Takatifu ya Bibi wa Karama Qum Ira. Katika hafla hiyo, alielezea vipengele mbalimbali vya utu wa mwanamke huyo mtukufu na kumtaja kuwa ni kielelezo cha subira, muqawama, kujenga matumaini na usimamizi wa hali za dharura.
Husseini, akirejelea aya isemayo:
«إِنَّمَا یُوَفَّی الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَیْرِ حِسَابٍ»
“Hakika wanaosubiri watapewa ujira wao bila ya hesabu”
Alisema kuwa: Bibi Zainab (s.a) ni miongoni mwa vielelezo mashuhuri zaidi vya subira na ustahimilivu katika historia ya Uislamu. Mwenendo wake unaonesha kwamba subira ya kweli haimaanishi kuvumilia matatizo pekee, bali pia inahusisha kudumisha imani na kusimama imara katika njia ya haki. Vilevile, neema na majukumu ya kidunia ni amana kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambazo zinapaswa kutumiwa katika njia iliyo sahihi.
Akizungumzia nafasi ya Bibi Zainab (s.a) baada ya tukio la Ashura, aliongeza kuwa; mwanamke huyo mtukufu alitekeleza jukumu muhimu katika mazingira magumu, kwa kuhakikisha usalama wa maisha ya Imam Sajjad (a.s) na kuandamana na msafara wa Ahlul-Bayt (a.s). Kupitia hotuba zake na juhudi zake za kutoa mwangaza na kufichua ukweli katika miji ya Kufa na Sham, hakuruhusu ujumbe wa mapinduzi ya Imam Hussein (a.s) usahaulike.
Mhubiri huyo wa Haram Takatifu ya Bibi wa Karama, akisisitiza umuhimu wa kumfsnya Bibi Zainab (s.a) kuwa kielelezo cha kuigwa, alielekeza umakini katika nyanja tatu za kimaadili na kiroho, uwajibikaji wa kijamii, pamoja na usimamizi wa familia na hali za dharura, alisema kuwa; imani, kumtegemea Mwenyezi Mungu, kujisitiri, kuwa na haya, kutetea haki na kuwajibika katika jamii ni miongoni mwa mafunzo muhimu zaidi yanayopatikana katika maisha ya mwanamke huyo mtukufu.
Husseini, akizungumzia namna Bibi Zainab (s.a) alivyokabiliana na kusimamia hali ngumu baada ya tukio la Ashura, alisisitiza kuwa; mwenendo wake unaonesha kwamba kuvuka nyakati za matatizo hakuhitaji subira na imani pekee, bali pia kunahitaji busara, kudumisha matumaini na kuwajibika, alieleza kuwa mafundisho hayo yanaweza kuwa mwongozo wenye manufaa katika maisha ya mtu binafsi, familia na jamii kwa ujumla.
Mwisho, akizungumzia nafasi ya wanawake katika malezi ya kizazi na shughuli za kiutamaduni, alisisitiza kuwa; kumfuata Bibi Zainab (s.a) kama kielelezo kunaweza kuchangia katika kuimarisha imani za kidini, kulea kizazi chenye ufahamu na uwajibikaji, pamoja na kueneza maadili mema katika jamii. Aidha, alieleza kuwa shughuli za kiutamaduni zinazofanyika shuleni, misikitini na katika vituo vya elimu zinapaswa kuambatana na uelewa wa hadhira inayolengwa na mazungumzo yenye mantiki na hoja za kuridhisha.
Maoni yako